Fursa ya kudhamini/kufadhili Tuzo za Ubora wa Elimu Tanzania (Tanzania Schools Academic Excellence Awards)

Fursa ya kudhamini/kufadhili Tuzo za Ubora wa Elimu Tanzania (Tanzania Schools Academic Excellence Awards)

TUZO ZA UBORA WA TAALUMA KWA SHULE ZA TANZANIA  (TANZANIA SCHOOLS ACADEMIC EXCELLENCE AWARDS)

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) kwa kushirikiana na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) imeandaa Tuzo zitakazojulikana kama Tuzo za Ubora wa Taaluma kwa Shule za Tanzania (Tanzania Schools Academic Excellence Awards) kuanzia mwaka 2019. Utoaji wa tuzo hizi ni jitihada za Serikali kutambua na kuwapongeza Wanafunzi, Waalimu, Shule, Halmashauri na Mikoa iliyoofanya vizuri katika Mitihani ya Taifa.

Tamasha la utoaji Tuzo litafanyika kila mwezi Machi kwa matokeo ya Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne (SFNA) na Kidato cha Pili (FTNA) pamoja na Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na kila mwezi Oktoba kwaMitihani ya Kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE) na Mtihani wa Kidato cha Sita (ACSEE). Tamasha la utoaji Tuzo litashirikisha Wizara, Taasisi za Serikali, Makampuni binafsi pamoja na wafanyabiashara wa Sekta mbalimbali.

LENGO LA UTOAJI WA TUZO

Lengo la tuzo hizi ni kutoa motisha itakayotoa hamasa kwa Wanafunzi, Waalimu, Shule, Halmashauri na Mikoa  kuongeza bidii na ubunifu wenye tija katika ufundishaji na ujifunzaji. Hii itasaidia kuongeza kiwango cha ufaulu, hivyo, kupata wahitimu wengi wenye ujuzi na maarifa ya kutosha kuiwezesha nchi yetu kufika katika uchumi wa viwanda.

Kudhamini/Kufadhili Bofya Hapa